Tuesday 18 July 2017

TRA yatoa kauli kuhusu William Ngeleja na Fedha za Escrow

Image result for Richard Kayombo
Waziri wa Nishati na Madini wa zamani William Ngeleja ni mmoja kati ya watu waliopokea mgawo wa fedha zinazodaiwa kuwa zao la kashfa ya Tegeta Escrow.


Siku Chache Baada Ya Mbunge Wa Sengerema, William Ngeleja (CCM), Kutangaza Kwa Umma Kuwa Amerejesha TRA Fedha Za Mgao Wa Tegeta Escrow Alizopata Tsh. 40.4 Milioni Na Kupewa Risiti, TRA Wameibuka Na Kusema Hawazitambui Fedha Hizo.

Mkurugenzi Wa Elimu Kwa Umma Wa TRA, Richard Kayombo Amesema Mamlaka Hiyo Inahusika Na Kuhakikisha Serikali Inakusanya Kodi Stahiki Na Siyo Urejeshwaji Wa Fedha Za Kashfa Kama Escrow.

"Fedha Za Escrow Zinaihusu Vipi TRA? Tunawezaje Kukaa Na Kuzungumzia Fedha Ambazo Si Zetu? Mimi Nashauri Watafutwe Wenyewe Wazungumze Kama Wanataka Kurejesha Lakini Siyo sisi "alisema Kayombo


e08eb46e-1b2d-4141-a0f3-f49132e24b6a.jpg
Payslip inayoonesha mrejesho wa fedha kutoka kwa Willliam Ngereja.

No comments:

Post a Comment