Simba imejipanga kufanya biashara kubwa ya jezi za wachezaji wawili wa kimataifa nao ni Emmanuel Okwi na Haruna Niyonzima.
Niyonzima raia wa Rwanda na Okwi kutoka Uganda wameishamalizana na Simba na wanachosubiri ni kuanza kazi tu.
“Jezi zao zitauzwa sawa na wengine lakini ni lazima kufanya oda kubwa ya jezi zao,” kilieleza chanzo.
Wachezaji hao watatambulishwa rasmi katika tamasha la Simba Day. Tayari maandalizi ya msimu mpya yameanza na Simba Hivi sasa iko Afrika Kusini.
No comments:
Post a Comment