Yanga imeendelea kufanya usajili
wa wachezaji wa ndani na nje ya nchi wakati huu wakirusha
Jiwe moja na kupiga ndege wawili Tayari viungo wawili (Mukoko
Tonombe na Tuisila Kisinda) kila mmoja amesaini
mkataba wa miaka miwili kujiunga na Yanga
wakitokea AS Vita ya Congo PR.
lakini hadi sasa bado haijulikani kocha wa timu hiyo ni nani.
Ratiba ya Ligi Kuu kwa msimu ujao inatarajia
kuanza mwezi ujao Septemba 6).
Amri Kiemba anasema kunaweza
kukawa na changamoto kwa Yanga kwa sababu klabu
imesajili wachezaji wengi wapya ambao wanakuja
kukutana na benchi jipya la ufundi.
"Kwa namna ambavyo siku zimebaki ili ligi kuanza na
hadi leo timu haina kocha mkuu wala msaidizi, ni
mtihani kwa klabu ya Yanga na vilabu ambavyo hadi
sasa hivi bado havija jua vitakuwa na kocha gani
msimu ujao."
"Kupanga ni kuchagua, haiwezekana kwa namna
ambavyo umechagua kufanya halafu ukategemea
matokeo ambayo yataletwa na kudra na Mwenyezi
Mungu kuliko ambavyo timu imejiandaa.”
"Yanga inawachezaji wengi ambao wameondoka (16)
kuna wachezaji wengi wapya wanakuja sasa
isijekuwa kikundi cha wachezaji badala ya timu."
"Faida kubwa kwa Yanga ingekuwa ni kuwa na kocha
msaidia ambaye alikuwepo kwenye timu msimu
uliopita hata kocha mpya akija anampa ripoti ya
kilichotokea msimu uliopita.
No comments:
Post a Comment