Saturday, 15 July 2017

Wayne Rooney kuondoka na watanzania wanne.

Image result for everton vs gor mahia
Baada ya juzi Alhamisi wachezaji wa Tanzania kukosa nafasi ya kupambana nyota wa zamani wa Manchester United ya England ambaye sasa anaitumikia Everton ya nchini humo, Wayne Rooney, Kampuni ya Mchezo wa Kubahatisha ya SportPesa inaandaa mpango kabambe kwa ajili ya wachezaji hao.

Rooney aliiongoza Everton kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Gor Mahia ya Kenya katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Uendeshaji wa SportPesa Tanzania, Abbas Tarimba amesema wanatarajia kuandaa mpango maalumu wa kuwasaidia wachezaji wa hapa nchini angalau wanne kila mwaka kwenda England kwa ajili ya kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa.

“Tunataka soka la Tanzania ilipige hatua ili siku moja na sisi tuwe na wachezaji wanaocheza  katika Ligi Kuu England.


 “Tunajipanga ili tuweze kuleta maskauti hapa nchini kwa ajili ya kuangalia wachezaji na ikiwezekana angalau kila mwaka Watanzania wanne waweze kwenda England kwa ajili kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa ili siku moja tuweze kuwaona wakipambana na akina Rooney katika ligi kuu ya nchi hiyo,” alisema Tarimba.

No comments:

Post a Comment