Monday, 14 August 2017

Cristian Ronaldo amjibu Lionel Messi

Cristiano Ronaldo celebrates scoring for Real Madrid by taking his shirt off and displaying it to the Nou Camp supporters 
Kama unakumbuka ilikuwa Aprili, mwaka huu pale Lionel Messi aliposhangilia baada ya kufunga bao mwishoni katika El Clasico kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu, Madrid, akaamua kushangilia kwa kuwaonyesha mashabiki wa Madrid jezi yake.

Messi aliionyesha jezi hiyo kwa mashabiki wa Madrid na kuzua gumzo, lakini leo Cristiano Ronaldo naye amejibu akiwaonyesha mashabiki wa Barcelona jezi namba 7, waisome baada ya kufunga bao la pili katika mechi ya Spanish Super Cup.

Madrid imeshinda kwa mabao 3-1 katika mechi hiyo lakini Ronaldo aliyeingia, alikumbana na red card baada ya kupata yellow mbili. Mechi ya pili dhidi ya timu hizo itakayopigwa Agosti 17 kwenye dimba la Santiago Bernabeu itaamua bingwa.



Baada ya kufunga bao hilo alivua jezi na kuwaonyesha mashabiki hao, sawasawa na alivyofanya Messi, Aprili, mwaka huu.

No comments:

Post a Comment