Afisa habari wa Klabu ya Simba Haji Manara ameanza majigambo yake mapya kwa kudai timu ya Yanga itaingia mitini katika mechi ya Ngao ya Jamii Agosti 23 kwa kuwa wanahofia watapigwa bao nyingi kutokana na kikosi walichokiona.
Manara amesema hayo, muda mchache ilipomalizika hafla yao ya kusherehekea siku yao maalum 'Simba day' ambapo walicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda na kuwafunga bao 1-0.
"Mimi ninachoogopa kwamba Yanga katika mechi ya Ngao ya Jamii hawatakuja kwa ule muziki waliyouona kutoka kwa wachezaji wetu. Mimi nawaambia mtakuja kusikia hapa watakizua kitu ili wakwepe mechi hiyo", amesema Manara.
Pamoja na hayo, Manara ameendelea kwa kusema "Nitawatabiria japo sifanyi kazi ya Shekhe Yahya lakini najua hawatafika kwa sababu wakija ni hatari watakuja kupigwa bao 7 au 8 halafu wapate aibu", amesisitiza Manara.
Kwa upande mwingine, Manara amesema wanatarajia kucheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Singida United Mjini Dodoma na Mtibwa Sugar katika mkoa wa Morogoro.
No comments:
Post a Comment