Wednesday, 23 August 2017

Hawa ndio watoto wa Tanzania waliofanikiwa kujiunga na Manchester City ya Uingereza.

Watoto wawili wa Kitanzania wenye umri wa miaka 12  Daudi pamoja na Malimi wameondoka jana usiku nchini na kuelekea nchini Uingereza kujiunga na Manchester City Academy.


Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. George Harrison Mwakyembe amefunguka na kusema kuwa kama vijana hao watafanikiwa katika majaribio hivyo watakuwa ni Watanzania wa kwanza kujiunga na Academy hiyo.

Wamekwenda kujiunga na Manchester City Academy kwa ufadhili wa kampuni ya TECNO Tanzania. Wakifaulu majaribio ya kujiunga, watakuwa Watanzania wa kwanza kujiunga na academy hiyo na baadaye kuchezea Manchester City" alisema Waziri Mwakyembe 

No comments:

Post a Comment