Wednesday, 23 August 2017

Polisi waenda kupekua nyumbani kwa Tundu Lissu.

Jeshi la Polisi limemaliza zoezi la kufanya upekuzi katika nyumba ya Mwanasheria Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) iliyopo Tegeta Dar es Salaam na baada ya hapo Lissu amerejeshwa Kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam.


Jeshi la polisi lilikwenda nyumbani kwa Tundu Lissu kufanya ukaguzi kufuatia makosa mawili ambayo Mbunge huyo wa Singida Mashariki na Rais wa TLS anatuhumiwa nayo ambayo ni pamoja na Kusema makosa ya Rais John Pombe Magufuli hadharani na chochezi kuhusu kushikiliwa ndege ya Tanzania aina ya Bombardier Q400 huko nchini Canada.

Kwa mujibu wa Afisa Habari wa CHADEMA, Tumaini Makene amedai kuwa Tundu Lissu amerudishwa  Kituo Kikuu cha Polisi kwa ajili ya taratibu zingine za kisheria ambazo zitaendelea ikiwa pamoja na dhamani ambayo kisheria ipo wazi. 
Tundu Lissu alikamatwa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2017 na jeshi la polisi alipotoka mahakamani kwenye kesi ya uchochezi , alipelekwa Police Central kwa ajili ya kufanyiwa mahijiano na baadaye kulala rumande kutokana na jana kushindwa kupewa dhamana. 

No comments:

Post a Comment