Saturday 19 August 2017

Haya ndio majibu yaliotolewa na Serikali kuhusu hoja ya Tundu Lissu.

Image result for tundu lissu
Serikali kupitia kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu Idara ya Habari, Zamaradi Kawawa imejibu hoja zilizotolewa na Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA Tundu Lissu kuhusu kushikiliwa kwa ndege ya Tanzania aina ya Bombadier Q-400 Dash 8 nchini Canada.


Zamaradi Kawawa amekiri kuwa ni kweli ununuzi wa ndege hizo umeingiliwa na mgogoro na kukiri kuwa ndege hiyo Q-400 Dash 8 inashikiliwa nchini Canada kwa madai ya kuwa ndege hiyo imeshikiliwa kwa mgogoro wa kutengeneza na wanasiasa wa Tanzania wasioitakia mema nchi ya Tanzania. 
"Ununuzi wa ndege ya 3 ya Bombadier umeingiliwa na mgogoro uliotengenezwa na wanasiasa na watu wasioitakia mema Tanzania, Wanasiasa waliotengeneza mgogoro huo wanahujumu maendeleo ya nchi na usalama wa raia"- alisema Zamaradi Kawawa
Aidha Zamaradi Kawawa amesema kuwa ndege ya tatu ambayo ilikuwa inatarajiwa kuingia nchini mwezi Julai amedai kuwa itaingia muda si mrefu na kuwataka Watanzania waiamini serikali ya Tanzania iliyopo chini ya Rais John Pombe Magufuli 
"Ndege ya 3 ya Bombadier ipo na inakuja kwahiyo wananchi waiamini Serikali yao ila serikali imesikitishwa na ushiriki wa wanasiasa na baadhi ya watu kuhujumu maendeleo ya nchi, Watanzania tuwe wazalendo kulinda, kutetea na kukabiliana na hujuma zozote zinazorudisha nyuma maendeleo ya Nchi, tuunge mkono jitihada za Rais Magufuli  katika kuleta maendeleo bila kujali itikadi ya chama, kabila au dini" alisisitiza Zamaradi Kawawa
Mbali na hilo Kawawa amesema kuwa serikali imeanza kuchukua hatua kadhaa kuhusiana na mgogoro wa ununuzi wa ndege hizo 
"Kuhusiana na mgogoro wa ununuzi wa ndege hatua za Kidiplomasia na sheria zimeanza kuchukuliwa ili kumaliza jambo hili" alisema Zamaradi Kawawa 
Hapo Jana Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia Na maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu katika taarifa yake kwa vyombo vya habari alisema ndege hiyo imeshindwa kuwasili nchini kufuatia kesi ya madai iliyofunguliwa dhidi ya Serikali ya Tanzania nakupelekea kukamatwa kwa Ndege hiyo mali ya 

No comments:

Post a Comment