Saturday 5 August 2017

Kamusoko atuma salamu kwa Simba na Niyonzima.

Image result for Thabani Kamusoko
Ungeweza kufikiri baada ya pacha wake, Haruna Niyonzima kuondoka, kiungo rasta wa Yanga Mzimbabwe, Thabani Kamusoko angeweza kuwa na hofu kubwa.

Lakini mambo ni tofauti kabisa, ameonyesha kujiamini zaidi na ametamba kikosi chao hivi sasa kipo fiti kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

Kauli hiyo, ameitoa mara baada ya kumaliza kambi ya mkoani Morogoro waliyoiweka kwa muda wa wiki mbili kujiandaa na ligi kuu iliyopangwa kuanza Agosti 26, mwaka huu. Pia kujiandaa na mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba Agosti 23, mwaka huu.

Kiungo huyo, wiki hii alijiunga na kambi hiyo akitokea kwao Zimbabwe alipokwenda muda mfupi baada ya kuongeza mkataba wa miaka miwili ya kuichezea timu hiyo.

Kamusoko alisema anafurahia kuona kila mchezaji akiwa fiti baada ya kumaliza mazoezi ya fitinesi kabla ya kurejea jijini Dar es Salaam, jana.

Kamusoko alisema, wamepanga kuendelea kulitetea tena taji lao la ligi kuu walilolichukua kwa misimu mitatu mfululizo chini ya kocha wao wa zamani Hans van Der Pluijm na baadaye Mzambia, George Lwandamina.

"Nawapongeza viongozi kwa kufanikisha kambi hii ya wiki mbili ya pamoja ya mazoezi ya fitinesi tuliyoiweka huku Morogoro.


"Kiukweli kabisa ukiangalia kila mchezaji unamuona yupo fiti kwa ajili ya mapambano, hivyo tunawaahidi mashabiki wetu kufanya vizuri katika msimu ujao,” alisema Kamusoko.

No comments:

Post a Comment