Friday 25 August 2017

Kocha wa Yanga Lwandamina aeleza ukweli kuhusu ishu ya kukatiwa tiketi ya ndege kurudi kwao

Image result for george lwandamina yanga
Baada ya mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba, taarifa zilidai kuwa Kocha wa Yanga, George Lwandamina alikatiwa tiketi ya ndege ya kuondoka Dar kwenda kwao Zambia, lakini kocha huyo amekanusha.

Taarifa za awali zilianza kusambaa baada ya kuonekana nakala ya tiketi ya Kampuni ya Fastjet ikionyesha kocha huyo anatarajia kuondoka leo Ijumaa saa 4:50 usiku kuelekea Zambia ambapo angefika kesho Jumamosi saa 6:20 usiku.

Tiketi hiyo ambayo inaonyesha namba ya ndege ambayo ni FN0250, inaonyesha jina la kocha huyo ambaye ndiyo msafiri na malipo yake yalitakiwa kufanywa jana Alhamisi kabla ya safari hiyo.


Uongozi wa Yanga ulikanusha taarifa hizo na alipotafutwa Lwandamina mwenyewe alisema: “Watu wengine huongea kwa niaba yangu.” Alipotumiwa nakala ya tiketi akajibu: “Hiyo ni tiketi bandia.”

No comments:

Post a Comment