Friday, 25 August 2017

Okwi aeleza mapya kuhusu Huruna Niyonzima.

Image result for emmanuel okwi katika ngao ya hisani
Kiungo mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi, ameibuka na kusema kuwa kiungo mwenzie Mnyarwanda, Haruna Niyonzima kiwango anachokionyesha uwanjani kitasaidia kuwapa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu utakapoanza kesho.

Ligi Kuu Bara inatarajiwa kuanza kesho Jumamosi ambapo Simba itafungua pazia dhidi ya Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

Okwi amesema kuwa Niyonzima, kwa uwezo wake alionao, atawasaidia mbio hizo za ubingwa kutokana na uzoefu wake na kuwa bado yupo katika kiwango bora.

No comments:

Post a Comment