Mahakama imetoa amri ya jengo la Yanga makao makuu ya klabu hiyo mitaa ya Kaunda na Jangwani kunadiwa.
Hii inatokana na deni la kodi ya Majengo la Sh milioni 300 ambalo klabu hiyo inadaiwa na Serikali.
Siku ya mnada imepangwa kuwa Agosti 19 yaani kesho kutwa kuanzia saa 4 asubuhi na Msolopa Investment ndiyo itakayohusika na mnada huo.
Hali hiyo inaonekana kuwashitua mashabiki wengi wa Yanga.
Juhudi za kuwapata viongozi wa Yanga zimekuwa ngumu kwa kuwa wengi hawakuwa wakipokea simu
No comments:
Post a Comment