Thursday, 17 August 2017

Kitila Mkumbo atema cheche kuhusu ishu ya Raila Odinga.

Image result for kitila mkumbo
Ikiwa imepita siku moja toka kiongozi wa upinzani Kenya (NASA) Raila Odinga kutangaza adhima ya umoja huo kwenda Mahakama ya Juu ya Kenya kupinga matokeo ya kura za urais yaliyompa ushindi Kenyatta, Kitila Mkumbo amempa shavu kwa maamuzi hayo.


Profesa Kitila Mkumbo ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji nchini Tanzania amesema kuwa maamuzi aliyofanya Odinga ni maamuzi sahihi na kudai kuwa Odinga ni baba wa Demokrasia katika ukanda wa Afrika Mashariki. 

"Ahsante sana Raila Odinga kwa hakika maamuzi uliyofanya kwenda mahakamani kutafuta haki ni maamuzi sahihi, wewe ni baba wa Demokrasia katika ukanda huu" alisema Kitila Mkumbo.
Aidha Kitila Mkumbo anamedai kipindi ambacho kina Odinga wanapambana kupigania mageuzi wakati wa muhula wa pili wa utawala wa rais Daniel arap Moi Uhuru Kenyatta yeye alikuwa kivulini.
"Huyu Kenyatta ni beneficiary. Wakati akina RAO wakipambana na akina Moi yeye alikuwa kivulini. Tuwe wa kweli" alisisitiza Kitila Mkumbo.
Matokeo rasmi ya IEBC ambao Odinga anayapinga yanaonyesha kuwa, Uhuru Kenyatta aliyegombea kwa tiketi ya chama cha Jubilee alipata ushindi baada ya kujizolea kura zaidi ya milioni nane na laki mbili sawa na asilimia 54.27 ya kura zote, huku Odinga aliyegombea kwa tiketi ya ODM akipata kura zaidi ya milioni 6 na laki saba, sawa na asilimia 44.74 ya kura zote.

No comments:

Post a Comment