Kesi iliyokuwa inawakabili Mkurugenzi wa kampuni ya VIP Engeneering na mmiliki mwenza wa zamani wa IPTL, James Rugemalira na Habinder Seth Sigh, imehairishwa mpaka Agosti 31 mwaka huu kutokana na upelelezi kutokamilika.
Maamuzi hayo yametolewa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na mwendesha mashtaka wa TAKUKURU, Leornad Swai ambapo alimueleza Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, hivyo anaomba kesi hiyo iahirishwe hadi tarehe nyingine.
Baada ya maelezo hayo ya Wakili Swai, Hakimu Mkeha aliahirisha kesi hiyo hadi August 31, 2017 ambapo washtakiwa wamerudishwa rumande.
Harbinder Singh Sethi pamoja na mfanyabiashara James Rugemarila kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 12, yakiwemo ya kutakatisha fedha na kuisababisha serikali hasara ya takribani Bilioni 309.
Kutokana na kesi hiyo kutokuwa na dhamana watuhumiwa hao wamerudishwa tena rumande mpaka tarehe 31 Agosti mwaka huu ambapo kesi yao itasomwa tena katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment