Thursday 17 August 2017

Hii ndio idadi ya shule zilizofungwa mpaka sasa kwa kukosa vigezo jijini Dar es salaam.

Image result for Profesa Joyce ndalichako.
Waziri wa Elimu,Sayansi Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako.
Manispaa ya Ilala imeendelea na zoezi la kuzufungia shule ambazo hazijasajiliwa katika Jimbo la Ukonga Dar es Salaam, ambapo inakadiriwa kuwa jumla ya shule 125 zitafungiwa.


Zoezi hilo linaloendeshwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, ambapo aamewataka wazazi wenye watoto katika shule zilizofungiwa kufika katika ofisi za manispaa hiyo kuthibitisha usajili wa shule.

Hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wenye shule wanaoendesha shule kinyume cha sheria, ambapo pia amewataka kufuata hatua za kiserikali katika kuendesha shule hizo.

Shule hizo zilizo fungwa ni shule za msingi na awali ambazo ziko chini ya sekta binafsi, Miongoni mwa shule zilizofungiwa ni pamoja na Mbingaa Nursery & Primary school English Medium, Montessori Nursery School & Proficience College Ilala.

No comments:

Post a Comment