Tuesday, 8 August 2017

Makamu wa Rais Samia Suluhu kuwa mgeni rasmi maonesho ya Nanenane.

Image result for Samia, Suluhu Hassan
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania, Mhe Samia, Suluhu Hassan leo anatarajiwa kuwaongoza Watanzania katika maadhimisho ya siku ya wakulima na Wafugaji nchini Tanzania ambapo kitaifa yatafanyika katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.

Katika Kilele hicho cha Nane Nane Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu, atatembelea mabanda mbalimbali yakiwemo ya Kilimo, Ufugaji na Uvuvi yaliyopo katika viwanja hivyo ikiwa ni pamoja na kuhutubia wananchi na wakulima na Wafugaji watakaojitokeza katika maadhimisho hayo.

Makamu wa Rais aliwasili Mkoani Lindi jana kwa ajili ya sherehe hizo na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi, Viongozi mbalimbali wa serikali, Wanachama wa Chama cha Mapinduzi na vikundi vya ngoma ambavyo vilimlaki kwa nyimbo mbalimbali.

Licha ya Sherehe hizo Kilele chake Kitaifa kufanyika Mkoani Lindi kwa Kanda ya Kusini Lakini Nyanda za Juu Kusini yatafanyika katika viwanja vya  John Mwakangale Mkoani Mbeya, Kanda ya kati ni Nzuguni Mkoani Mbeya, Kanda ya Kaskazini yatafanyika jijini Arusha na Kanda ya Mashariki yatafanyika mjini Morogoro.

No comments:

Post a Comment