Tuesday, 1 August 2017

Rais Magufuli amuapisha Balozi Mashiba na kupokea hati za Utambulisho wa mabalozi.(+picha)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo amemuapisha Mhe. Benedict Martin Mashiba kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi


Mhe Benedict Martin Mashiba amechukua nafasi ya Mhe. Victoria Richard Mwakasege ambaye amestaafu nafasi hiyo, mbali na hilo Rais Magufuli amepokea hati za utambulisho wa Mabalozi watano walioteuliwa kuziwakilisha nchi zao hapa nchini. 

Mbali na hilo Rais Magufuli amewapongeza mabalozi hao kwa kuteuliwa kuziwakilisha nchi zao hapa nchini na kuwaomba mabalozi hao kutilia mkazo diplomasia ya Uchumi kwa kuongeza juhudi za kuhamasisha wafanyabiashara na wadau wengine wa maendeleo kushirikiana na Tanzania katika biashara na miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwepo ujenzi wa viwanda, Kilimo na huduma za jamii. 
Mabalozi waliowasilisha hati zao za utambulisho ni
1.    Mhe. Nguyen Kim Doahn – Balozi wa Vietnam hapa nchini. 
2.    Mhe. Prof. Ratlan Pardede – Balozi wa Indonesia hapa nchini. 
3.    Mwadhama Askofu Mkuu Marek Solcynski–Balozi wa Vatican hapa nchini. 
4.    Mhe. Dkt. Detlef Wachter – Balozi wa Ujerumani hapa nchini. 
5.    Mhe. Richard Tumisiime Kabonero – Balozi wa Uganda hapa nchini.



Habari Picha

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli  akimuapisha Benedict Mashiba kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Tanzania nchini Malawi Benedict Mashiba akila kiapo cha uadilifu kwa Viongozi mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Malawi Benedict Mashiba mara baada ya tukio la uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli  akipokea Hati za utambulisho kutoka kwa Balozi wa Vietnam hapa nchini Nguyeni Kim Doahn, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Vietnam hapa nchini Nguyeni Kim Doahn akipigiwa wimbo wa Taifa mara baada ya kuwasili Ikulu kwa ajili ya kuwasilisha Hati za Utambulisho.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli  akiagana na Balozi wa Vietnam hapa nchini Nguyeni Kim Doahn mara baada  ya kumaliza mazungumzo pamoja na kupokea Hati za Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Vietnam hapa nchini Nguyeni Kim Doahn katikati akipigiwa wimbo wa Taifa mara baada ya kuwasili Ikulu kwa ajili ya kuwasilisha Hati za Utambulisho.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli  akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Indonesia hapa nchini Prof. Ratlan Pardede, Ikulu jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Indonesia hapa nchini Prof. Ratlan Pardede, Ikulu jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli  akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Vatican hapa nchini Mhashamu Askofu Mkuu Marek Solcynski, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli  akimshukuru Balozi wa Vatican hapa nchini Mhashamu Askofu Mkuu Marek Solcynski mara baada ya kupokea Hati zake za Utambulisho Ikulu jijini.
Balozi wa Ujerumani hapa nchini Dkt. Detlef Wachter akipigiwa wimbo wa Taifa mara baada ya kuwasili Ikulu kwa ajili ya kukabidhi Hati zake Utambulisho.
Balozi wa Ujerumani hapa nchini Dkt. Detlef Wachter akijitambulisha kabla ya kuwasilisha Hati zake za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Ujerumani hapa nchini Dkt. Detlef Wachter mara baada ya kupokea hati zake za Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli  akipokea Hati za utambulisho kutoka kwa Balozi wa Uganda hapa nchini Richard Tumisiime Kabonero Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli  akipiga ngoma ya Brass Bendi ya Jeshi la Polisi ambayo ilifika Ikulu kwa ajili ya mapokezi ya Mabalozi mbalimbali kutoka nje ya nchi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Brass Bendi ya Jeshi la Polisi Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

No comments:

Post a Comment