Klabu ya Mtibwa Sugar imefanikiwa kuinasa saini ya mshambuliaji wa Taifa Stars Kelvin Sabato ‘Kevy Kiduku’, kutoka Majimaji FC alikocheza msimu uliopita ikiwa zimebaki siku chache kufungwa kwa dirisha kuu la usajili kwa msimu mpya wa mwaka 2017/2018.
Sabato amesaini rasmi mkataba wa miaka miwili jana jioni, kujiunga na Mtibwa Sugar ambayo bado inajisuka upya kwa ajili ya msimu ujao.
Hayo yamewekwa wazi na taarifa zilizotolewa na uongozi wa klabu hiyo huku wakisema wanafuraha kubwa kufanikiwa kunasa saini ya mshambuliji huyo nguli wa Taifa Stars.
No comments:
Post a Comment