Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limesema mechi ya watani Yanga na Simba, itaanza saa 11 jioni. Awali mechi hiyo ya Ngao ya Jamii, ilipangwa kuanza saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, kesho kutwa Jumatano. Lakini Msemaji wa TFF, Alfred Lucas ametangaza mabadiliko hayo ya ratiba ya mchezo huo kusogezwa kwa saa moja zaidi.
No comments:
Post a Comment