Tuesday, 22 August 2017

Tundu Lissu Mikononi mwa Jeshi la polisi.

Related image
Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA Tundu Lissu amekamatwa na polisi leo wakati akitoka Mahakama ya Kisutu na kupelekwa Central Police jijini Dar es Salaam


Afisa habari wa CHADEMA Tumaini Makene amethibitisha kukamatwa na Tundu Lissu 

"Tumetoka Mahakama ya Kisutu muda huu ambapo Mwanasheria Mkuu wa Chama, Tundu Lissu alikuwa na kesi ya tuhuma za uchochezi (uchochezi one) lakini pia alikuwa ni wakili kwenye kesi inayomkabili Yericko Nyerere hapa hapa Kisutu. 

Wakati gari la Lissu likiwa liko getini tayari kwa kutoka, likawa blocked na nyuma ya gari yake pia likasimama gari jingine likiwa na askari polisi wenye silaha, kisha wengine wakamfuata na kumwambia yuko chini ya ulinzi na atakiwa kwenda Central Police" alisema Tumaini Makene .

Makene aliendelea kusema baada ya hapo polisi hao walimtaka ashuke kwenye gari yake na kuingia kwenye gari ya polisi kwa ajili ya kwenda Central Police 

Tundu Lissu amekamatwa leo tarehe 22 Agosti 2017 zikiwa zimepita siku tatu toka alipotoa taarifa ya ndege ya Tanzania  'Bombadier Dash Q400' kuzuiliwa nchini Canada kutokana na amri ya mahakama

No comments:

Post a Comment