1.Ukiingia
nyumbani kwake ukaona anampigia simu yule dada wa usafi
anaye kujaga mara moja kwa wiki aje kufanya usafi alipwe usidhani eti anakujali
kiivyo laasha hana kutesiti tu aone kama utasema "acha baby nitakufuria tu
ucjali mpenz wangu. Uvivu na kujali
2.Ukikuta kwake
amefanya shopping ya vyakula vya kupika kama mchele, unga, maharage, samaki,
mafuta na vingine kibao tu halafu anakuambia muende mgahawani mkale dinner my
friend usizani eti hana pesa nyingi sana za kutumia."Anakutesti aone kama
utamwambia mbaki kwake mpike mle. Fahamu Uko chumba cha mtihani ujue.
3.Ukimtembelea kwake
ukamkuta anapika au anafanya usafi halafu wewe unaenda kukaa unaanza kuagalia
movie halafu ukitaka kumsaidia anakuambia endelea tu baby kuangalia movie
usijali karibu namaliza ,eti na wewe unarudi kwenye kochi miguu juu kwenye sofa
unaendelea na movie yako.. "Siku zako zinahesabika
4.Ulishawai kumwambia
mpenzi wako aende kwenye ibada ? Alipo kataa ulimsisitiza "Ndugu yangu hata walevi wanapenda wanawake wanao
wasisitiza kwenda kumuomba mungu. "Nikamtihani anakupa.
5.Mara ngapi huwa
unamkumbusha kuwaombea dua wazazi wake kama wapo hai au hata kama wametangulia
mbele ya haki AU kumkumbusha kuwajulia
hali wazazi wake pamoja na kuwatumia pesa za matumizi "Huo ni mtihani
mwingine wakuwa nao makini
6.Jifunze pia kujisiri
mwili wako usipende kuacha mwili wako wazi kila wakati hasa ukiwa matembezini
au kwenye shughuli zako na pia ukiwa kwake pendelea kukaa karibu yake uwe una
mbusu kila atakapo ongea neno nzuri la kufurahisha.
7.Jaribu ukiwa unaenda
kwake nenda na tuvitu vitu kama nyanya, vitunguu, na mafuta hivyo vyote wanaume
ni shida sana kununua.
8.Wakati mwingine nenda
kwake na CD za dini au hata flash yako unaweka mawaidha yanayo mzungumzia Mungu
msikilize wote sio wewe kila ukifika kwake wewe ni movie kwenda mbele na music
tu sijui wa kina Diamond, jux na Vanessa
ukiwa wa hivyo hata hona tofauti yako na wale macho juu juu anao kutana nao
club.
9]Jaribu kumshauri
kuhusu kufanya biashara zaidi ya moja yani kuwekeza zaidi , lakini hata kuanzia
kufikiria kuhusu kesho kwa mfano ukamwambia unaonaje mpenzi wangu ununue shamba
au kiwanja. Wanaume wengi wanapenda mwanamke anaye waza mbali na kufikiri zaidi
nje ya Box.
10.Tengeneza utaratibu
wako na yeye kwa kuwatembelea watoto yatima na kuwasaidia wahitaji tofauti
katika jamii.
No comments:
Post a Comment