Monday, 28 August 2017

Yaliyojiri katika Kesi ya Jamhuri dhidi ya JamiiForums - Oilcom kuhusu Uchakachuaji/Ukwepaji kodi bandarini.


IMG_6119.JPG
Kesi dhidi ya JamiiForums inayohusiana na Kampuni ya Oilcom na Uchakachuaji Mafuta imesogezwa mbele kupisha Jamhuri kufanya marekebisho ya Mashitaka kwa mara nyingine. 

Kesi hiyo sasa itatajwa tena Septemba 26, 2017,ambayo itakuwa ni mara ya 3 kwa kesi hii kufanyiwa marekebisho.

Mara ya mwisho upande wa Jamhuri ulidai umekamilisha taratibu zote na ukaomba tarehe 28 na 29 Agosti ili waje na mashahidi zaidi watakaotoa ushahidi wao dhidi ya JamiiForums.

Tayari shahidi wa kwanza kwenye kesi hii alishafanyiwa mahojiano na kutoa ushahidi wake. Alikuwa ni kaimu ZCO, Ndg. Ramadhani Kingai .

[​IMG]

Wakili aliyesimama upande wa JamiiForums, Ndg. Peter Kibatala ameonekana kukerwa na danadana inayochezwa na Jamhuri katika kesi hii. Wakili Tundu Lissu amesema atahakikisha tarehe 26 Septemba anakuwepo mahakamani ili ashirikiane na wenzake kujua hatima ya kesi hii.

REJEA YA MADA TAJWA:
USHUHUDA: Hivi ndivyo mafuta yanavyoibiwa Bandarini Dar 
na USHUHUDA: Hii ndiyo michezo hatarishi ya Kampuni ya Mafuta ya Oilcom.
=====


Shahidi anasema anaikumbuka barua ile aliiona kwa macho yake na anaiomba aitoe mahakamani kama kielelezo. Shahidi anaambiwa aisome barue.

Wakili anamuuliza shahidi ana maoni gani kuhusu barua kutoka Jamiiforums, Shahidi anasema yeye hajaona taarifa yoyote ya faragha katika zile walizoomba.

Anaendelea kuwa tarehe 01/04/2016 waliandika barua nyingine kukumbushia taarifa hizo na walinukuu kifungu cha 10 subsection 2-8 ya Crime Procedure Act.

Kifungu hicho kinawapa mamlaka polisi kupata taarifa kutoka ofisi yoyote kama taarifa iko relevant na suala linalofanyiwa upelelezi. Baada ya barua hiyo JamiiForums hawakujibu tena, hivyo tukaona kuwa wanadhoofisha upelelezi wetu tukaamua tuwakamate wakurugenzi.

Anaulizwa lini walichukua uamuzi wa kuwakamata?
Anajibu baada ya kuwa wamefungua shauri.

Una lingine la kuongezea?
"Mheshimiwa sina"
===========

Sasa anaingia wakili Tundu Lissu na anasema ana maswali mengi sana.

Tundu Lissu Anasema aeleze kisomo chake mpaka amekuwa SSP wa polisi

Shaidi anasema: 2001 May aligraduate CCP kama constable wa polisi, 2002 feb-july 2003 alipata Assistant inspector. 2006 December, ass inspector to full inspector wa polisi. 2009 Feb-July alienda mafunzo ya uofsa na kuwa ASP wa polisi. 2014 akiwa katika ulinzi wa amani Sudan alipanda from ASP to SSP. Mwaka jana ndo akawa SSP

Tundu Lissu : kwa maelezo yako ni sawa nikisema wewe ni afisa wa polisi mwenye uzoefu wa upelezi wa makosa ya jinai?
Jibu: Ndio

Tundu Lissu : Ni sahihi kuwa una uzoefu wa upelelezi ndani na nje ya nchi?
Jibu; Ndio

Tundu Lissu: Kwa mujibu wa maelezo yako taarifa ya Usama Mohammed ndio ilipelekea mfungue jalada?
Jibu: Ndio

Tundu Lissu: Na ndio zilipelekea muandike barua kwa JF 23 February 2016?
Jibu: Kweli

Tundu Lissu: Naomba umueleze hakimu kama hiyo barua iko mahakamani.
Jibu: Haipo.

Tundu Lissu: Sasa shahidi mimi ninayo hiyo barua(Anampa shahidi na kumwambia aiangalie).
Tundu Lissu: "Angalia hiyo barua SSP Kingai"

Tundu Lissu Anamwambia amwambie mheshimiwa hakimu kama ile barua imeandikwa kwa Maxence Melo.
Jibu: Haijataja jina la mtu

Tundu Lissu: Kwahiyo jina la Max Melo Mubyazi halipo?
Jibu: halipo

Tundu Lissu: Je! Imeelekezwa kwa Mike William?
Jibu: haijataja jina

Tundu Lissu: Sasa naomba useme kama kwenye hiyo barua mmesema kuwa mmepata taarifa toka kwa Usama Mohammed?
Jibu: hatujaandika na hatukuwa na sababu ya kufanya hivyo.

Tundu Lissu
: Jamiiforums ni kampuni??
Jibu: Ni kampuni

Tundu Lissu: Kama ni kampuni inatakiwa aiandikishwe brela, hati ya kuandikishwa brela iko wapi?
Jibu: Mheshimiwa mimi natoa ushahidi kama mtoa maelekezo, walioandika hizo barua watakuja na kueleza.

Tundu Lissu: Nauliza iko wapi? Yaani iko mahakamani sasa?
Jibu: Ndio

Tundu Lissu: Kama kampuni inatakiwa iwe na Memorandum of Association, iko wapi?
Jibu: Sifahamu

Tundu Lissu: Inatakiwa iwe na Bodi ya Wakurugenzi...ipo?
Jibu: Sifahamu

Tundu Lissu: Nilikusikia ukisema mliwaandikia wakurugenzi ili wawape taarifa, ulimaanisha nini kama sasa unasema haujui kama ina bodi ya wakurugenzi??
Jibu: Mimi najua Wakurugenzi, bodi sijui.

Tundu Lissu: Una ushahidi wa aina yoyote kutoka brela kuhusu JF kama kampuni na washtakiwa kama wakurugenzi.
Jibu: kwa sasa sina ushahidi

Tundu Lissu Kampa ile hati ya mashtaka, anasema aeleze kama kuna sehemu wanasema kama walipata taarifa kutoka kwa Usama Mohammed.
Jibu: Hakuna

Tundu Lissu: Naomba useme kama kuna sehemu mmesema kuwa mlikuwa mnachunguza taarifa zinazohusu ukwepaji kodi au kuiibia serikali.
Jibu: Hapana

Tundu Lissu: Taarifa za ukwepaji kodi za Fahrer mliziprint??
Jibu: sijui kama ziliprintiwa

Tundu Lissu: Kwa hiyo ziko wapi?? Wewe si ndio kiongozi wa upelelezi
Jibu: Hazipo mahakamani kwa sasa.

Tundu Lissu: Unataka hakimu azifate shimoni?
Jibu: Mimi ni shahidi mmoja kati ya wengi wengine watakuja nazo.

Shahidi amesoma barua toka kwa wanasheria wa JF. Kipande kimoja kinasema "mteja wetu yuko tayari kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi kwa mujibu wa sheria"

Tundu Lissu anamuuliza sasa " ulisema kuwa katika barua hiyo JF ilijibu kuwa ina wajibu wa kulinda faragha za wateja wao. Kwa ufahamu wako kuna haki ya kila mtu kulindiwa faragha ya mawasiliano yake au hakuna?"
Jibu: Inategemea

Tundu Lissu: Haki ipo au haipo??
Jibu: Kwa private person sifahamu...

Tundu Lissu: Kwa ufahamu wako kuna haki ya kulindiwa faragha ya mawasiliano kwa kila mtu including private persons?
Jibu: Sifahamu

Tundu Lissu: Barua ile ya kutoka kwa wanasheria wa JF inasema " mteja wetu anaomba ufafanuzi wa sheria itumikayo kuomba taarifa za mteja" kwa uelewa wako mtu anayeomba ufafanuzi amekataa kutoa taarifa au hajakataa?
Jibu: Kwa maelezo hayo amekataa.

Tundu Lissu: Mtu anayeandika kuwa " mteja wetu angependa kujua kipi cha sheria kinatumika kuomba taarifa za mteja ukiacha kifungu namba 32 cha Cyber Crime Act" Mtu aliyeuliza ni kifungu kipi cha sheria kinatumika amekataa kutoa taarifa au hajakataa?
Jibu: Kwa maelezo hayo ya sasa hajakataa.

Tundu Lissu: Umesema baada ya kupokea barua ya kutoka kwa wanasheria wa JF mliandika nyingine 1/4/2016...je iko mahakamani?
Jibu: Sina uhakika nadhani ipo mahakamani.

Hakimu: mimi sina.

Tundu Lissu: Mimi ninayo

Hakimu: Haiwezi kutumika wakati mimi sina haijafika mahakamani.

Tundu Lissu: Inaweza tumika Sababu ameitaja.

Tundu Lissu: Mweleze hakimu kama barua imewataja watuhumiwa.
Jibu: Haijawataja.

Tundu Lissu: Kwenye ushahidi wako wa msingi umesema kuwa barua hii haikujibiwa si ndio?
Jibu: Sijui kama haikujibiwa.

Tundu Lissu: Wewe ni msimamizi gani wa upelelezi usiyejua taarifa muhimu.
Jibu: Sikupata taarifa kama imejibiwa

Tundu Lissu katoa barua toka kwa Victory attorneys iliyojibu barua ile ya 01/04/2016.

Tundu Lissu: Shahidi tafadhali ieleze mahakama kama barua hiyo haina mhuri wa kupokelewa na ofisi ya mkuu wa upelelezi kanda maalum ya Dar
Jibu: Sina uhakika na Barua hii na wala Mhuri sina uhakika nao.

Tundu Lissu: Naomba uulinganishe mhuri huo na ule wa kwenye exhibit PI (barua ya majibu ya mwanzo)
Jibu: Mimi sio expert wa hayo mambo siwezi kulinganisha.

Tundu Lissu: Tusomee hiyo document imeandikwa kupokewa lini
Jibu: Kwa mujibu wa document hiyo inaonesha ilipokewa 06/05/2016

Wakili wa serikali anaobject hapo Kuwa, shahidi hawezi kuendelea kuhojiwa kwa document asiyokuwa na uhakika nayo.

Tundu Lissu: Naomba barua hii iwe admitted in evidence for purposes of impeaching the witness....(itumike kama kielelezo cha kumvua ushahidi shahidi husika)

Upande wa serikali: Shahidi aliyesimama mahakamani ameletwa na jamhuri, kumuimpeach shahidi ni kwa yule aliyemwita mahakamani....Lissu hawezi kumuimpeach shahidi aliyeletwa na jamhuri. Purpose of cross examination ni kucheck credibility ya shahidi...hawatakiwi kumuimpeach...wasubiri muda wa defence kutumia hizo documents...shahidi hawajamleta wao. Au wanipe kifungu wanachotumia kutaka kumuimpeach shahidi.

Tundu Lissu anatoa kifungu...Hakimu anapelekewa akisome 164 (1).

Baada ya kusoma hicho kifungu, Hakimu Kasema kesho Muda wa saa nne asubuhi kesi itaendelea.

Chanzo:JF

No comments:

Post a Comment