Thursday 7 September 2017

Jeshi la Polisi limetoa tahadhari kwa mashabiki kuhusu Mechi ya Azam FC VS Simba.

Related image
Jeshi la Polisi Tanzania limetoa tahadhari mapema kwa wale ambao hawatakuwa na tiketi za mechi kati ya Azam FC dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa Azam Complex, keshokutwa.

Ofisa wa masuala ya michezo katika jeshi hilo, Hashim Abdallah amesema ulinzi utakuwa mkali.

“Kama hauna tiketi baki nyumbani, huu ni msisitizo. Vizuri ukabaki nyumbani maana ulinzi utakuwa mkali na hatutatoa nafasi kwa watakaotaka kufanya fujo.

“Mara baada ya uwanja kujaa, mara moja milango itafungwa,” alisema kwa msisitizo.

Taarifa zinaeleza pamoja na askari, kutakuwa na mbwa pamoja na farasi ambao watahusika na ulinzi.


Uwanja huo una nafasi ya watu 7,000 waliokaa vitini hali ambayo imelalamikiwa na mashabiki wengi wa soka nchini.

No comments:

Post a Comment