Thursday 7 September 2017

Kesi ya Jamal Malinzi mahakama yasogezwa mbele.

Kesi inayomkabili aliyekuwa Rais wa shirikisho la Mpira wa Miguu(TFF), Jamal Malinzi na wenzake wawili imeahirishwa hadi Septemba 21 baada ya hakimu anayesikiliza shauri hilo kuwa na dharura.


Hayo yameelezwa na Wakili wa serikali, Faraj Ngokah mbele ya Mahakama ya Kisutu Jijini Dar es Salaam na kusema upelelezi wa kesi hiyo hujakamalika pamoja na Hakimu anayesikiliza shauri hilo, Wilbard Mashauri amepatwa na dharura.

Kutokana na hayo, Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa ameahirisha kesi hiyo hadi Septemba 21 mwaka huu itakapotajwa kwa mara nyingine tena.

Kwa upande mwingine, viongozi hao wanatuhumiwa na makosa mbalimbali  yakiwemo ya matumizi mabaya ya madaraka waliyokuwa nayo katika uongozi wao pamoja na kughushi na kutakatisha fedha kupitia akaunti ya TFF.

No comments:

Post a Comment