Thursday 7 September 2017

Kocha Joseph Omog aendelea kuunda Simba ni ya Magoli.

Image result for Joseph Omog
Kocha Joseph Omog amezidi kwa mara nyingine kusisitiza katika soka la kushambulia mfululizo.

Katika mazoezi ya Simba, Omog amekuwa akisisitiza suala la kushambulia mfululizo.


Mmoja wa wachezaji wa Simba amesema, Omog sasa anachotaka ni mabao mengi.
“Wengi hawajui kocha katumia muda mwingi sana kuujenga mfumo wa ulinzi kwa kuwa hataki kabisa kufungwa.

“Lakini sasa msisitizo wake ni mabao tena ikiwezekana ni mengi ingawa suala la nidhamu ya kulinda analisisitiza sana,” alisema.

Simba tayari imeanza Ligi Kuu Bara kwa ushindi wa mabao 7-0 katika mechi dhidi ya Ruvu Shooting.


Mechi inayofuata ni dhidi ya Azam FC wikiendi hii kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment