Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Zanzibar), Salum Mwalimu amefunguka na kusema kwamba wanawaruhusu Chama cha Mapinduzi watumie nafasi ya Lowassa kuwepo Chadema kuwaita wao mafisadi kama jinsi wao walivyofanya kwa miaka mingi.
Salumu amesema kwamba kuwataja watu ambao waliwaita vinara wa ufisadi na leo wapo nao kwenye chama chao ulikuwa ni wajibu wao kama chama cha upinzani kutumia upenyo wa udhaidfu wa chama cha mapinduzi kuonyesha wananchi madhaifu ya serikali.
"Lazima ukubali kwamba ni wajibu wetu kuonyesha madhaifu ya serikali, Kama tulikuwa tunampinga Lowassa kwamba ni fisadi ulikuwa ni wajibu wetu Chadema. Sasa kama leo hii Lowassa yupo kwetu ni wajibu wao CCM kuwaambia watanzania kuwa Chadema kina mafisadi. Kwa sababu Lowassa amekuja Chadema ni yule yule wala hajawa malaika kama jinsi ambavyo kelele zinavyopigwa," Mwalimu amefunguka
Akizungumzia kuhusu chama kupwaya na kumtegemea mtu mmoja kuwa mkosoaji wa serikali iliyopo Madarakani, Mwalimu amesema kupanga ni kuchagua hivyo wao kama Chadema wanauwezo mkubwa wa kukosoa lakini huamua kuchagua nani atoe hoja kwa wakati gani na siyo kwamba wameishiwa.
"Hata kwenye timu ya mpira wapo mastaa wengi wanaofanya vizuri lakini huangaliwa ni nani wa kuibeba timu, ndivyo hata Chadema ilivyo, mnaweza kuwa wengi lakini kupanga ni kuchagua, Tundu ni Mwanasheria Mkuu wa chama hivyo chama kinaanda ajenda lakini atachaguliiwa mmoja wa kuifikisha ajenda hiyo huku wengine tukitoa sapoti, inategemea ajenda hiyo pia inatolewa wakati gani, mbona hapa katikati mengine yametokea kwani tumemuinua Lissu kitandani atusaidie kusema. si tulisema wenyewe. ? hivyo hakuna mtu mmoja anayeibeba Chadema bali tunashirikiana pamoja", Mwalimu ameoneza.
Huu ni utaratibu wetu hata kipindi cha kina Mh. Zitto Kabwe pamoja na Dkt. Slaa wote agenda zilikuwa ikitengenezwa na watu ndani ya chama na wanaozipeleka mbele huwa ni wachache siyo kwamba eti chama kimepwaya.
Katika hatua nyingine Mwalimu amesema lengo la chama cha upinzani ni kushika dola na siyo kusikiliza jinsi ambavyo watu wengine wanavyokosoa na kusisitiza kwamba Chama chao kilianzishwa kwa malengo ya kuja kushika dola.
No comments:
Post a Comment