Thursday, 19 October 2017

Kocha wa Yanga Lwandamina azungumza maneno yake kuhusu hali ya Pius Buswita.

Image result for Pius Buswita
Mwendo alioanza nao kiungo wa Yanga, Pius Buswita, umeonekana kuwa "mguu mzuri" kwa kuwa Kocha wake, George Lwandamina amevutiwa.

Buswita ambaye amesajiliwa Yanga msimu huu akitokea Mbao FC, katika mechi sita za Ligi Kuu Bara ambazo timu yake imecheza mpaka sasa, amefanikiwa kucheza mbili kutokana na awali kufungiwa.

Ikumbukwe kuwa, wakati Buswita anasajiliwa na Yanga, ilibainika kwamba alisaini kwanza Simba, hali ambayo ilisababisha Kamati ya Maadili na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kumfungia kwa muda wa mwaka mmoja kutokana na kosa hilo.

Hata hivyo Yanga ilifanya juhudi za kumtoa kifungoni, ndipo kamati hiyo ikamtoa kwa sharti la kulipa kwanza shilingi milioni kumi ambazo zilitajwa kwamba ndizo alizozichukua wakati anasaini Simba. Zikalipwa akaanza kucheza.

Akizungumzia kiwango cha Buswita ambaye amecheza dhidi ya Mtibwa Sugar na Kagera Sugar, Lwandamina amesema: 

“Pius amekuwa na kiwango kizuri tangu aanze kucheza hapa, ni mchezaji mzuri ambaye ataisaidia timu. Kikubwa anatakiwa kuendelea na kasi hii hadi mwisho.”

No comments:

Post a Comment