Wednesday, 25 October 2017

Jamhuri Kihwelo awapa maneno ya angalizo Simba kuhusu Ibrahim Ajibu wa Yanga.

Image result for Jamhuri Kihwelo
Kocha wa Dodoma FC ya Mkoani Dodoma, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ameitaka timu yake ya zamani ya Simba kuwa makini na  mshambuliaji wa Yanga, Ibrahim Ajibu, Jumamosi katika mechi ya Ligi Kuu Bara kati ya Simba na Yanga.

Jumamosi kuna mchezo wa Simba na Yanga na mashabiki wamekuwa wakiusubiri kwa hamu kubwa kuona ni timu gani inaweza kuibuka na ushindi.

Julio ambaye ni mchezaji wa zamani wa Simba na kocha wa timu hiyo amesema kuwa Simba wanatakiwa kumlinda sana mshambuliaji huyo kwa kuwa sasa amebadilika siyo kama zamani.

Julio alisema, mchezo huo unatarajia kuwa mgumu na wenye upinzani wa hali ya juu na kuwataka Simba wasiibeze Yanga kwa kuwa ina kikosi kizuri na wanacheza mpira wa kueleweka.

“Ajibu ni mchezaji mzuri ana kiwango cha hali ya juu sio yule aliyekuwa Simba, hivyo ni mchezaji wa kuchungwa sana katika mchezo huo, naamini mchezo huo utakuwa mgumu na wenye upinzani wa hali ya juu.

“Simba wanahitaji kuwa makini na siyo kama nasema vibaya ila naamini kutakuwa na ushindani mkubwa katika mechi hiyo ijapokuwa naamini mechi itakuwa na ugumu wa hali ya juu  kutokana na kila upande kujiandaa ipasavyo.


“Mechi hii mara nyingi huwa inakuwa haina mwenyewe kutokana na kila upande kujiandaa vyema kuelekea mchezo huu hivyo tunasubiria siku ya Jumamosi,” alisema Julio.

No comments:

Post a Comment