Wednesday 25 October 2017

Tetesi za soka kutoka barani Ulaya .

Image result for Carlo Ancelotti
Everton inamtaka aliyekuwa kocha wa Real Madrid na Chelsea Carlo Ancelotti kwenda kuingia katika ligi ya Uingereza na kuwa mkufunzi wake mpya, hatahivyo kocha huyo ambaye ni raia wa Itali anamtaka Mkufunzi wa Swansea Paul Clement kuwa naibu wake, (Sun)

Everton imemchagua aliyekuwa kocha wa zamani wa Borrusia Dortmund Thomas Tuchel kuwa chaguo lao la kwanza baada ya kumfuta kazi kocha Ronald Koeman. (Daily Mirror)
Everton inataka kuipiku Leicester kumsajili kocha wa Burnley kuwa mkufunzi wake mpya (Daily Express)
Dyche
Image captionDyche
Dyche analengwa na Everton na anaweza kuwagharimu £2.5m kama fidia, huku chaguo jingine likiwa mkufunzi wa timu ya Everton ya vijana wasiozidi miaka 23 David Unsworth kuchukua kazi hiyo hadi mwisho wa msimu. (Telegraph)
David Unsworth anatarajiwa kuifunza Everton kwa muda lakini yeye anataka kuifunza timu hiyo kwa muda mrefu.(Guardian)
Mkufunzi wa Watford Marco Silva
Image captionMkufunzi wa Watford Marco Silva
Mkufunzi wa Watford Marco Silva ndio chaguo la Jamie Carragher's kumrithi Ronald Koeman katika timu ya Everton (Daily Telegraph)
Ronald Koeman alikuwa amesita kuzungumza na wachezaji wake kabla ya kufutwa kazi kama mkufunzi wa timu hiyo. (Times - subscription required)
Kiungo wa kati wa zamani wa Argentina Matias Almeyda, ambaye ndio mkufunzi wa timu ya Guadalajara nchini Mexico anawania kuwa mkufunzi wa Leicester (Mirror)
West Ham inamtaka mkufunzi mkuu wa klabu ya Hoffenheim Julian Nagelsmann kuchukua mahala pake Slaven Bilic. (Daily Express)
Image captionWest Ham inamtaka mkufunzi mkuu wa klabu ya Hoffenheim Julian Nagelsmann kuchukua mahala pake Slaven Bilic. (Daily Express)
West Ham inamtaka mkufunzi mkuu wa klabu ya Hoffenheim Julian Nagelsmann kuchukua mahala pake Slaven Bilic. (Daily Express)
Wachezaji wa West Ham walifanya mkutano muhimu katika uwanja wao wa mazoezi kufuatia kushindwa na Brighton, huku kocha wao Bilic akikabiliwa na shinikizo kali kuhusu kazi yake. (Daily Mail)
David Moss ameondoka katika klabu ya Huddersfield Town baada ya miezi mitano kama mkuu wa operesheni (Independent)
Arsene Wenger hatma yake kujulikana Alhamisi
Image captionArsene Wenger hatma yake kujulikana Alhamisi
Mkufunzi Arsene Wenger na bodi ya Arsenal zitatakikana siku ya Alhamisi katika mkutano mkuu wa kila mwaka kufanya maamuzi ya mwisho kuhusu hatma ya ukufunzi wa klabu hiyo kabla ya miwsho wa msimu ujao.(Daily Telegraph)
Jose Mourinho alitoa na kurusha koti lake katika sakafu wakati alipokuwa akiwakosoa wachezaji wake katika chumba cha kujiandaa kwa mara ya kwanza katika ukufunzi wake baada ya klabu hiyo kushindwa na Huddersfield siku ya Jumamosi. (Sun)
Usain Bolt
Image captionUsain Bolt
Waziri wa michezo Tracey Crouch ametishia kukata ufadhili wa shirikisho la soka Uingereza FA na kulizuia kutowania kuandaa mashindano makubwa hadi pale shirikisho hilo litakapojiimarisha kufuatia tetesi zinazomzunguka Eni Aluko. (Daily Telegraph)
Mtu mwenye kasi zaidi duniani ,Usain Bolt, anapigania kucheza soka ya kulipwa lakini ''hatojiaibisha'' katika kufanya hivyo. (Daily Mail)
Kiungo wa kati wa Liverpool Philippe Coutinho, 25, anasema kuwa kikosi hicho ni sharti kijiimarishe haraka iwezekanavyo katika safu yake ya ulinzi kufuatia kushindwa kwao 4-1 na Tottenham hotspurs. (Daily Star)

No comments:

Post a Comment