Yanga iko mjini Shinyanga kuivaa Stand Unite na sasa uhakika haitamtumia Thabani Kamusoko na ameendelea kubaki jijini Dar es Salaam.
Kwa kuwa Kamusoko hakwenda Shinyanga, maana yake inaonekana Kocha George Lwandamina ameamua kumpa mapumziko ya kutosha ili afanye maandalizi kwa ajili ya mechi ijayo dhidi ya Simba.
Imeelezwa, Lwandamina anataka Kamusoko awe fiti Yanga itakapoivaa Simba Oktoba 28.
Awali ilielezwa, Kamusoko angeenda mjini Shinyanga kuungana na kikosi cha Yanga baada ya kuachwa jijini Dar es Salaam pamoja na Donald Ngoma.
Lakini Kamusoko amebaki jijini Dar es Salaam akiendelea na matibabu ili kuhakikisha anakuwa fiti.
No comments:
Post a Comment