Monday 23 October 2017

TFF yaweka hadharani dau la kuiona mechi ya Simba na Yanga Siku ya Jumamosi.

Image result for simba na yanga ngao ya jamii 2017
Shirikisho la soka nchini TFF limetangaza 

viingilio vya mchezo wa ligi kuu soka Tanzania 

VPL, raundi ya nane kati ya wenyeji Yanga SC 

dhidi ya Simba siku ya Jumamosi kwenye 

uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.




Taarifa kutoka shirikisho imebainisha kuwa watazamaji watakaotaka kuketi kwenye jukwaa kuu watapaswa kulipia shilingi elfu ishirini 20000/= ili kuona mchezo huo wa watani wa Jadi.

Watazamaji watakaoketi eneo la mzunguko watalipia shilingi elfu kumi, 10000/= ili kushuhudia mchezo huo unaotarajiwa kuwa na mvuto wa kipekee kutokana na aina ya wachezaji walisajiliwa msimu huu wa 2017/18.

Yanga na Simba zitaingia uwanjani zote zikiwa na alama 15, Simba ikiwa juu kwa tofauti ya mabao hivyo mshindi wa mchezo huo ana nafasi kubwa ya kuongoza ligi huku akisubiri matokeo ya Mtibwa Sugar dhidi ya Singida United.

No comments:

Post a Comment