Monday, 23 October 2017

Zitto Kabwe aibua jipya baada ya kauli ya Rais Magufuli hii leo kuhusu Bombardier.

Related image
Mbunge wa Kigoma Mjini na kiongozi wa Chama Cha ACT Wazalendo amefunguka na kusema kuwa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi ya awamu ya tano imekopa dollar milioni 500 kutoka benki ya Uswiss na pesa hizo ndiyo zimetumika kulipa ndege za Tanzania. 

Zitto Kabwe amesema hayo leo kupitia mitandao yake ya jamii na kusema kuwa riba ya mkopo huo ni mkubwa sana na kudai watu wa chini wakiwepo wavuvi wa Migebuka kutoka Kigoma watahusika kulipa deni hilo kupitia kodi zao. 

"Serikali ya CCM ya awamu ya Tano imekopa $500m kutoka Benki ya Credit Suisse ya Uswiss Kwa riba kubwa Sana. Sehemu ya fedha hizo zimetumika kulipia ndege ambazo Serikali inanunua. Wavuvi wa Migebuka Kigoma watahusika kulipa deni hilo kupitia kodi zao" alisema Zitto Kabwe 
Rais Magufuli leo amesema kuwa uchumi wa nchi unazidi kukuwa na kudai serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ina pesa za kutosha ndiyo maana imeweza kununua ndege mpya zaidi ya sita kwa mara moja na kudai watu ambao wanasema uchumi umeshuka wanaichonganisha serikali na wananchi. 

No comments:

Post a Comment