Monday 6 November 2017

Antonio Conte afunguka sababu ya kutompa nafasi David Luiz katika mchezo wao na Manchester United.

Chelsea defender David Luiz could face a lengthy spell out of their squad
Meneja wa Chelsea Antonio Conte amesema hafahamu iwapo beki David Luiz atasalia Stamford Bridge.

Mchezaji huyo wa miaka 30 hakujumuishwa kwenye kikosi cha Chelsea dhidi ya Manchester United Jumapili na hata hakuwekwa kwenye benchi.
Badala yake, meneja huyo alimchezesha Andreas Christensen.
Alipoulizwa kumhusu Luiz, Conte alisema: "Lazima atie bidii la sivyo atakuwa kwenye benchi au kwenye viti vya mashabiki."
Luiz was dropped for Chelsea's Premier League win over Manchester United on Sunday
Kuhusu mustakabali wa Luiz, Conte aliongeza: "Sijui, Christensen ndiye sasa na siku za usoni kwa Chelsea."
Lakini inasemekana mchezaji huyo alionesha kutilia shaka mbinu za maandalizi za Conte kabla ya mechi.
Image result for david luiz with antonio conte
Mbrazil Luiz amecheza dakika 90 katika kila mechi za Chelsea tatu walizokuwa wamecheza karibuni Ligi ya Premia na alicheza walipolazwa 3-0 na Roma Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya katikati ya wiki.
Lakini Jumapili, aliketi nyuma ya benchi ya Chelsea, akiwa amejifunga skafu ya rangi nyeusi kichwani.
The risk paid off as Chelsea won 1-0, and after the game Conte praised the players who came in
Alirejea mara ya pili Chelsea kwa £34m kutoka Paris St-Germain Agostit 2016 na alikuwa kwenye kikosi kilichoshinda ligi msimu uliopita.

No comments:

Post a Comment