Monday 6 November 2017

Taarifa kamili kuhusu Said Ndemla kuelekea kucheza soka nchini Sweden.

Image result for ndemla wa simba
Kiungo wa Simba Hamis Said Juma (Ndemla) ataondoka nchini kesho kuelekea nchini Sweden kwaajili ya majaribio ya kucheza soka la kulipwa nchini humo.


Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo mchana huu imeeleza kuwa Ndemla amepata nafasi ya kufanya majaribio katika klabu ya  AFC Eskilstuna inayoshiriki ligi kuu ya Sweden.

Majaribio hayo yatakuwa ya siku 14 ambapo tayari klabu imempatia ruhusa mchezaji huyo ambaye kipaji chake kililelewa kwenye timu ya vijana na klabu hiyo.

Ndemla amekuwa hapati nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha kocha Joseph Omog lakini klabu yake ipo tayari kumpokea na kuendelea na majukumu yake endapo hatafuzu japokuwa klabu imesema katika taarifa yake kuwa ina imani atafuzu.

No comments:

Post a Comment