Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Freeman Mbowe amedai kwamba Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF anayetambuliwa na msajili wa vyama Prof. Ibrahim Lipumba kuwa ni Profesa wa ajabu ambaye anaweza kubomoa chama alichokijenga.
Akiwa kwenye kampeni za uchaguzi mdogo Mtwara, Mh. Mbowe amesema kwamba hana ugomvi wowote na Prof Lipumba ingawa amekiri atakuwa muongo akisema kwamba anamuheshimu kwani anatumika katika kukivuruga chama alichokuwa akikiongoza kwa muda mrefu.
Mh. Mbowe amesema kwamba wakati CUF ikishirikiana na UKAWA kwa ujumla kutafuta kura na kuongeza wabunge wa chama hicho bungeni, yeye Prof Lipumba alikuwa mafichoni na anamshanga sasa hivi anavyorudi ndani ya chama hicho na kutaka kukisambaratisha.
"Sina ugomvi na Prof Lipumba lakini nikisema namuheshimu nitakuwa muongo sana. Prof Lipumba ni msomi sana tena msimchezee kwenye elimu lakini usomi ni jinsi unavyotumia elimu yako lakini siyo wingi wa vyeti. Ni Profesa wa ajabu kweli kweli. Mimi simuogopi mtu nitazungumza straight. Amesema Mbowe
Pamoja na hayo Mbowe amedai kwamba Spika wa Bunge pamoja na Msajili wa vyama vya siasa wanatumika katika kuibomoa CUF na kuongeza kwamba hataacha kusema ukweli kwani hakuna mtu yoyote anayemuogopa isipokuwa Mungu pekee.
Ameongeza kwamba kasi inayotumika kuibomoa CUF inatumika pia kuibomoa CHADEMA na kuweka wazi kwamba siku chama cha Chadema kikiuliwa labda awe amefariki lakini siyo wakati huu ambao bado anapumzi.
No comments:
Post a Comment