Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imemhukumu muigizaji wa Filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ kifungo cha miaka miwili jela baada ya kukutwa na hatia ya kumuua Steven Kanumba, tukio lililotokea April 7, 2012, Sinza Vatican jijini Dar es Salaam.
Kabla ya hukumu hiyo, wakili wa upande wa utetezi, Peter Kibatala alipopewa nafasi ya kumtetea mteja wake na Jaji Sam Rumanyika aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo, alisema kwamba Lulu anategemewa na familia yake nakwamba wakati tukio hilo linatokea, alikuwa bado mdogo.
Hivi ndivyo mlolongo wa kesi ulivyokuwa kuanzia asubuhi alipowasili mahakamani hapo.
Muigizaji wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amekutwa na hatia ya kuua bila kukusudia ambapo hukumu itatolewa baada ya mawakili wake kujitetea
#UPDATE: Wakili Kibatala anamtetea Lulu kwamba wakati tukio linatokea, alikuwa bado mtoto na jamii inamtegemea.
#UPDATE: Jaji Sam Rumanyika amemtia hatiani msanii Elizabeth Michael ‘Lulu’ kwa kosa la kuua bila kukusudia na sasa amemtaka wakili wa upande wa utetezi, kama ana ombi lolote la kupunguziwa adhabu.
#UPDATE: Jaji Sam Rumanyika amesema kifo kilitokana na ugomvi hivyo amejiridhisha kwamba mtuhumiwa aliua bila kukusudia. Jaji ameongeza kwamba wivu wa mapenzi ni maangamizi.
#UPDATE: Jaji Sam Rumanyika anayesikiliza kesi hiyo, anaendelea kusoma vifungu mbalimbali vya kisheria vinavyohusiana na kesi ya Lulu, muda wowote kuanzia sasa, hukumu itasomwa.
No comments:
Post a Comment