Katika dakika chache zilizopita , spika wa bunge la Zimbabwe ametangaza kuwa rais Robert Mugabe amejiuzulu .
Spika wa bunge Jacob Mudenda alisema kuwa hatua hiyo ni ya kujitolea na amefanya hivyo ili kuweza kuwepo kwa mabadiliko mazuri ya mamlaka kulingana na chombo cha habari cha reuters.
Tangazo hilo la ghafla lilizuia harakati za bunge kutaka kumng'oa madarakani ambazo zilikuwa zimeanza dhidi yake.
Wabunge walifurahia kufuatia hatua hiyo na raia wameanza kusherehekea barabarani.
Awali bwana Mugabe alikuwa amekataa kujiuzulu licha ya jeshi kuchukua mamlaka huku hatua hiyo ikifuatiwa na maadamano ya raia waliotaka kiongozi huyo kung'atuka mamlakani wiki hii.
No comments:
Post a Comment