Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola analenga kumnunua Riyad Mahrez katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari (Don Balon via The Sun)
Nahodha wa zamani wa klabu ya West Brom Derek McInnes, anayeisimamia Aberdeen, ni miongoni mwa wagombea wa kuchukua mahala pake mkufunzi wa klabu hiyo aliyefutwa kazi Tony Pulis kama mkufunzi. (The Scottish Sun)
Hatahivyo mashabiki wa West Brom wanamtaka mkufunzi wa zamani wa Everton kuchukua mahala pake Pulis. (Express & Star)
Mkufunzi wa zamani wa klabu ya West Ham Alan Pardew, meneja wa zamani Nigel Pearson na mkufunzi wa timu ya Ireland Martin O'Neill ni miongoni mwa wakufunzi walioorodheshwa katika kuchukua kazi ya meneja wa West Brom job. (Guardian)
Mkufunzi wa zamani wa Uingereza Sam Allardyce pia analengwa kuichukua kazi ya ukufunzi wa klabu ya West Brom na imebainika kwamba baadhi ya wachezaji wa klabu hiyo walikuwa wakitaka mkufunzi Pulis kuondoka. (Mirror)
Pulis ni miongoni mwa wakufunzi wanaopigiwa upatu kumrithi Paul Clement iwapo Swansea itamfuta kazi na pia atakuwa miongoni mwa wale wanaopigania kazi ya kuifunza Wales. (Daily Telegraph)
Mchezaji wa zamani wa Liverpool Dirk Kuyt anaamini mchezaji wa Uholanzi Virgil van Dijk ni mchezaji mzuri anayefaa kujiunga na klabu hiyo ya Anfield. (Sky Sports via Express)
Philippe Coutinho alimpiku Robbie Fowler na Michael Owen baada ya kutoa usaidizi wa goli la 31 la Liverpool siku ya Jumamosi.
Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Manchester United Andy Cole amietaka klabu yake ya zamani kumzuia mshambuliaji wa Ufaransa Anthony Martial, huku akidai kwamba Marcus Rashford ana uwezo mkubwa wa kuimarika zaidi. (ESPN)
Kwengineko mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho amepigwa jeki kufuatia habari kwamba Bayern Munich wamejiondoa katika kumwania mshambuliaji wa Atletico Madrid Antoine Griezmann, 26. (Daily Star)
Kiungo wa kati wa Arsenal na Ujerumani Mesut Ozil, 29, anasakwa na klabu ya Schalke, klabu ambayo alianza kushiriki soka ya kulipwa .(Kicker - in German)
Mshambuliaji wa Watford na raia wa Brazil Richarlison, 20, anasakwa na baadhi ya vilabu nchini China baada ya kufunga mabao 12 katika mechi 12 za ligi ya Uingereza. (Watford Observer)
Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp amekataa kumuuza Daniel Sturridge, 28, katika soko la uhamisho la mwezi Januari. (Liverpool Echo)
Kipa wa Liverpool na Wales Danny Ward, 24, na mshambuliaji Ben Woodburn, 18, wanatakiwa na mkufunzi mpya wa Sunderland Chris Coleman. (Sunderland Echo)
Celtic huenda ikamuania beki wa klabu ya Reading mwenye umri wa miaka 24-Liam Moore mnamo mwezi January. (Reading Chronicle)
No comments:
Post a Comment