Friday, 3 November 2017

Kocha Mkuu wa Simba Omog asema neno kuhusu kiwango cha Mkude.

Image result for Joseph Omog na jonas mkude
Kocha Mkuu wa Simba, Mcameroon, Joseph Omog amesema kuwa kitendo cha kiungo wake, Jonas Mkude cha kuonyesha kiwango cha juu katika mechi Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga, sasa anaweza kumuanzisha katika mchezo wa Jumapili dhidi ya Mbeya City.

Endapo, Mkude atafanikiwa kuanza katika mechi ijayo basi hiyo itakuwa ni mara yake ya tatu kuanza kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo tangu kuanza kwa msimu huu.

Mechi ya kwanza kuanza katika kikosi cha kwanza msimu huu ilikuwa ni dhidi ya Mwadui FC kisha Mtibwa Sugar. Michezo mingine yote aliyocheza alikuwa akianzia benchi.

Omog alisema kutokana na uwezo ambao Mkude amekuwa akiuonyesha kila anapoingia uwanjani hususan dhidi ya Yanga bila shaka anaweza kumwanzisha dhidi Mbeya City, siku ya Jumapili.

“Mkude hivi sasa yupo vizuri na amekuwa akionyesha kiwango cha juu kila mechi anayocheza, hata hivyo kuna vitu nimevibaini kwa hiyo naweza kumwanzisha katika mechi yetu na Mbeya City,” alisema Omog.

Simba itapambana na Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, mchezo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani Mkubwa.

No comments:

Post a Comment