KOCHA Mkuu wa Yanga, Mzambia, George Lwandamina, amesema kuwa, anataka kuona wanapata ushindi kwenye mchezo wao wa kesho Jumamosi dhidi ya Singida United, ili kujiimarisha zaidi kwenye nafasi yao ikiwezekana kukaa kileleni.
Lwandamina ameyasema hayo wakati kesho Jumamosi kikosi chake kitakapokuwa wageni wa Singida United katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa kwenye Uwanja wa Namfua mkoani Singida.
Yanga ambayo kwa sasa ina pointi 16 sawa na Simba, inashika nafasi ya pili kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa ambapo ushindi kwenye mchezo huo, utaifanya timu hiyo kukaa kileleni ikisubiri matokeo ya keshokutwa Jumapili kati ya Mbeya City na Simba.
“Ligi bado haijachanganya sana, lakini kwa hali ilivyo sasa, kupoteza pointi ni pigo kubwa, hivyo tutahakikisha katika mchezo ujao tunaondoka na pointi zote tatu ili kujiimarisha kwenye msimamo,” alisema Lwandamina.
No comments:
Post a Comment