Saturday, 4 November 2017

Kocha wa Mbeya City Nsanzulwimo Ramadhan afunguka yake kuhusu Simba.

Image result for Nsanzurwimo Ramadhan mbeya cityKocha wa Mbeya City, Nsanzulwimo Ramadhani raia wa Burundi amewataka wachezaji wake kutowafikiria Simba kama timu kubwa katika mchezo wao wa kesho ndani ya Uwanja  wa Sokoine jijini Mbeya huku akisema hawatatumia miguu yote 24 kwa wakati mmoja hata kama wao ni wakubwa.

Simba na Mbeya City zinatarajiwa kukutana kesho katika Uwanja huo huku Simba ikiwa na kumbukumbu ya msimu uliyopita ikiwalaza kwa bao 2-1.

Nsanzulwimo amewaambia hayo wachezaji wake muda mfupi baada ya mazoezi yao kumalizika katika uwanja huo asubuhi ya leo.

"Kama mpo tayari kushinda katika mchezo wetu wa kesho dhidi ya Simba naomba msifikirie  fedha za usajili wao kwani hautacheza na badala yake wanaocheza ni wachezaji kama nyinyi wenye miguu sawa na nyinyi. 

"Nitafurahi sana mkijiamini kwa kutokua na wasiwasi juu yao na mkacheza kama ilivyo kwa mechi zingine zilizopita tutapata matokeo mazuri," alisema Nsanzulwimo.


Pia Nsanzulwimo amesikitishwa na kitendo cha kumkosa kipa wake namba moja, Owen Chaima kutokana na kupewa taarifa za kufungiwa na Bodi ya Ligi ya TFF.

No comments:

Post a Comment