Monday 27 November 2017

Meya wa Ubungo Jacob Boniface aeleza sababu ya kukamatwa na Polisi.

Image result for Jacob Boniface
Meya wa Manispaa ya Ubungo kupitia CHADEMA Jacob Boniface ambaye jana alishikiliwa na polisi, ameweka wazi sababu ambayo jana ilimsababishia kukamatwa na jeshi la Polisi na kulala ndani, huku uchaguzi ukiendelea.


Meya Jacob amesema yeye alikuwa ni msimamizi wa vituo vya kupigia kura ambayo ipo kisheria, lakini baada ya muda alishangaa kuona polisi wanakuja kumkamata kwa tuhuma ambazo hazikuwa za kwlei.

“Nilikuwa nasimamia uchaguzi kama msimamizi wa uchaguzi wa chama changu, nikiwa kituoni nashangaa kuona nakuja kukamatwa na polisi, nilipofika kule wakaniambia kuwa wamepata taarifa kwamba nimejipanga kufanya vurugu na wenzangu, kitu ambacho sio kweli”, amesema Jacob Boniface.

Meya huyo ambaye ni miongoni mwa viongozi machachari wa CHADEMA amesema mpaka sasa hajajua hatma yake kama anapelekwa mahakamani au la, kwani aliachiwa huru majira ya saa saba usiku baada ya kulipa dhamana, huku uchaguzi ukiwa umeshakwisha.

No comments:

Post a Comment