Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye amesema CCM ni chama bora kuliko vyama vyote nchini na kwa sababu hiyo hawezi kukihama.
Nape amesema ndani ya CCM kuna Itikadi, sera, umoja, mshikamano wa kweli, kukosoana bila unafiki, kusahihishana na kanuni ya nitasema kweli daima, fitina kwangu ni mwiko inakubaliwa. huwezi kupata nafasi kama hizi katika vyama vya upinzani kwa sababu wenyeviti wake wanahodhi vyama.
Ameyasema hayo wakati akimnadi mgombea udiwani wa Kata ya Reli, Genfrid Mbunda katika uwanja wa Manispaa ya Mtwara Mikindani.
“Unajuwa wapinzani wasipoteze muda wa kusubiri mimi lini nitahama CCM badala yake wafanye kazi ya kuvijenga vyama vyao kwa sababu walitamani sana muziki huu uhamie kwao ndio maana wanabaki wanapiga kelele za kuwapa presha wanaCCM hivyo sitahama kwa sababu ukinikata mwili wangu damu yangu unakuta CCM,” alisema Nape
Nape alienda mbali zaidi na kusema, ‘’Kutokana na kanuni ya nitasema kweli daima, niliwahi kumwambia fisadi mmoja anaitwa Edward Lowassa ambaye alitaka kutuchakachua jengo la umoja wa vijana, nikamwambia, Mzee hebu kuwa na breki kidogo acha utapeli’’
Amewaambia wananchi wasibabaishwe na kundi la vyama vya upinzani kwa sababu hawana uwezo kiuongozi lakini pia CCM ndiyo iliyopewa ridhaa ya kuongoza nchi kupitia ilani yake ya Uchaguzi na kinachofanyika kwa sasa ni kujaza nafasi tu ya kiongozi atakayewasemea wananchi serikalini kupitia Ilani ya Uchaguzi ya CCM.
No comments:
Post a Comment