Monday 27 November 2017

Rais mstaafu Kikwete atoa pongezi kwa Rais Magufuli.

Image result for Jakaya  Kikwete NA MAGUFULI
Rais mstaafu wa serikali ya awamu ya nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amempongeza rais wa awamu ya tano Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwezesha elimu bure.


Dkt. Kikwete amesema hayo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa ‘Twitter’ baada ya kuweka video iliyomwonesha akizungumza na watoto wa kijiji cha Mangae mkoani Morogoro.
‘Nikiwa njiani kutokea Iringa kurudi Dar es Salaam nimekutana na watoto katika kijiji cha Mangae mkoani Morogoro. Nimefarijika kuwa wote wako shule. Ni matokeo ya elimu bure. Nampongeza Rais @MagufuliJP kwa kuwezesha watoto hawa kuwa shule”, amendika Kikwete.
Pongezi hizo za mstaafu Kikwerte kwenda kwa rais Magufuli zimekuja ikiwa ni siku moja tu tangu rais Magufuli ampongeze na kumshukuru rais mstaafu kwa kuwezesha ujenzi wa Hospitali na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kampasi ya Mloganzila jijini Dar es salaam.

 “Watu tunapenda sifa lakini hizi sifa sio zangu ni za rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwani mimi nilikuwa naagizwa tu nikiwa waziri wa Ujenzi, ndio maana nimeona niseme wazi kuwa sifa zote zimwendee mzee Kikwete”, alisema rais Magufuli kwenye ufunguzi wa Hospital hiyo.

No comments:

Post a Comment