Kiungo wa Simba, Said Ndemla, jana alifanikiwa kupanda ndege kwenda nchini Sweden katika timu ya AFC Eskelistuna kwa ajili ya kufanya majaribio ya siku 14. Na anatarajia kutua jijini Stockholm, leo.
Kiungo huyo amefanikiwa kuondoka baada ya safari yake hiyo kukwama Jumanne iliyopita kutokana na tatizo la usafiri.
Hivi karibuni, Ndemla alipata ofa nchini Sweden katika timu ya AFC Chiben, lakini ofa hiyo iliyeyuka hivyo kuendelea kuwa na majukumu ya kuitumikia timu yake ya Simba.
Alipoulizwa juu ya safari hiyo, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara alisema: “Ndemla anaondoka leo (jana) jioni kuelekea Sweden kwa ajili ya majaribio yake ya siku 14 kama tulivyosema.”
AFC ndiyo timu anayochezea Mtanzania, Thomas Ulimwengu ambaye hata hivyo, ameendelea kukaa nje kutokana na kuandamwa na majeraha.
No comments:
Post a Comment