Thursday 9 November 2017

Serikali yatoa ufafanuzi ilipofikia kuhusu swala la Tundu Lissu kupigwa risasi.

Image result for tikisa media tundu lissu
Imeelezwa kuwa Serikali bado inaendelea na uchunguzi wa matukio kadhaa ya uhalifu yanayoendelea kutokea nchini ikiwemo shambulio lililofanywa dhidi ya Mbunge wa Singida mashariki, Tundu Lissu.


Kauli hiyo imetolewa na Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa, wakati akijibu swali la kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni Freeman Mbowe ambaye alihoji ni kwanini Serikali imekataa kutoa kibali cha wao kuleta wachunguzi wa kimataifa ili kufatilia matukio ambayo yamekuwa yakitokea nchini na kuhatarisha amani ikiwemo suala la Lissu
Image result for kassim majaliwa bungeni
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

“Mheshimiwa Mbowe bado tuna imani na vyombo vya dola nchini, hivyo basi tuvipe muda ili wakamilishe upepelezi wa matukio hayo na mengine mengi nchini ili wakamilishe kazi yao kwa ufanisi”. Alisema Waziri Mkuu.

Mbowe aliendelea kuhoji swali la nyongeza kuwa anaomba Waziri mkuu amueleze kuna ugumu gani kuruhusu uchunguzi kwa vyombo vya kimataifa na kudai kuwa si kwamba hana imani na vyombo vya ndani bali anahisi kuwa havina dhamira ya kuchunguza tukio hilo na upande wake ndio wenye maumivu.

Waziri mkuu amejibu kuwa hakuna aliyefurahishwa na tukio la mbunge Lissu kupigwa risasi, na kama Mbowe akitaka majibu zaidi ya hayo, asubiri ripoti ya vyombo vya dola kwani ndio vyenye jukumu hilo.

Aidha Waziri Mkuu ameongeza kuwa Amani ndio tunu ya Tanzania ni wajibu wa  kila mmoja kuhakikisha anailinda kwa manufaa ya wote hivyo basi uchunguzi huo hauwezi kuwa wa jana na leo Jeshi lipewe muda lije na taarifa yenye manufaa.

No comments:

Post a Comment