Wednesday 8 November 2017

Tetesi zote za Soka kutoka barani Ulaya.

Image result for Mesut Ozil
Mshambuliaji wa Arsenal Mesut Ozil, 29, amesema kuwa atasaini mkataba mpya ikiwa klabu hiyo itammpa namba 10 ya Jack Wilshere. (Sun)

Meneja wa wa Atletico Madrid, Diego Simeone, ndiye lengo kuu la mmiliki wa Everton, Farhad Moshiri kuwa meneja mpya wa Everton. (Sky Sports)
Image result for Juan Mata
Real Madrid wanampango wa kumwinda mechezaji wa safu ya kati wa Mancester United Juan Mata mwezi Junuari. (Daily Express)
Mchezaji wa safu ya kati wa Machester United Marouane Fellaini, 29, anatafutwa na klabu ya Uturuki ya Besiktas ambao watajaribu kumsaini mwezi Januari.
Mesut OzilHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMesut Ozil
West Ham watahitaji kuwauza baadhi ya wachezaji wake wachanga, akiwemo mlinzi Reece Oxford, 18, na mchezai wa safu ya kati Josh Cullen, 21, ili kumsaini meneja mpya David Moyes. (Daily Mirror)

Arsenal inajaribu kumsaini mchezaji wa kiungo cha kati wa Besiktas raia wa Uturuki, Oguzhan Ozyakup, miaka mitano tangu wamuuze kwa klabu hiyo ya Uturuki kwa paunia 400,000. (Fotomac, via Metro)
NeymarHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionNeymar
Tottenham wanajiandaa kusaini mchezaji wa safu ya kati wa Besiktas Tolgay Arslan ,27, kwa kima cha pauni milioni 8.8.
Mabinga wa Ufaransa Paris St-Germain wana nia ya kumteua meneja wa Manchester United Jose Mourinho kuongeza uwezekano wa Neymar kusalia klabuni. Neymar 25 amehusishwa na kuhama kwenda Real Madrid. (Don Balon via Daily Express)
Newcastle United wameonyesha nia ya kumsaini mshambuliaji wa L;iverpool Danny Ings, 25, kwa mkopo mwezi Januari. (Newcastle Chronicle)
Matumaini ya Arsenal ya kumsaini mchezaji wa kuingo cha kati wa Barceloona Arda Turan, 30, yameongezeka baada kuambia kuwa anaweza kuondoka mwezi Januari. Sport, via Daily Mail)

No comments:

Post a Comment