Chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kimepata pigo baada ya kuondokewa na wanachama 50 mkoani Geita ambao wamehamia Chama cha Mapinduzi (CCM).
Vijana hamsini wanachama wa CHADEMA kutoka kijiji cha Buligi kata ya Senga wilayani Geita wamekihama chama hicho na kujiunga na CCM wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani.
Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Katibu wa UVCCM wilayani Geita Bw. Ali Rajab alisema vijana hao wamehama Chadema na kujiunga na CCM kutokana na kasi ya utendaji ya Rais Magufuli.
Katika kampeni hizo Bw. Rajab amewataka watumishi kuacha kufanya kazi kwa mazoea ili kuendana na kasi ya Rais Magufuli na Chama cha Mapinduzi CCM kwa ujumla kwani bila kufanya hivyo .
Naye Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa wanawake, UWT wilayani Geita Bi. Mazoea Salim, amesema CCM inatarajia kushinda kwenye uchaguzi huo mdogo katika kata ya Senga kutokana na uwezo wa mgombea ambaye wamemsimamisha.
No comments:
Post a Comment