Uongozi wa Yanga umesema unataka wachezaji wanaojituma na wenye nia ya kuisaidia klabu.
Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amesisitiza kwamba wale wachezaji wanaotanguliza fedha badala ya kupambana kwa ajili ya klabu hawatakuwa na nafasi.
Charles Boniface |
“Atakayeleta sintofahamu atachukuliwa hatua. Sisi tunahitaji mchezaji ambaye amelenga kuisaidia klabu,” alisema.
“Kama lengo lake litakuwa ni fedha pekee na anapanga kutuvuruga basi tutaachana naye.
“Lakini nasisitiza, tunahitaji wachezaji walio fiti ambao watakisaidia kikosi chetu. Kama tutaona mchezaji ni majeruhi kwa muda mrefu tutaachana naye.”
No comments:
Post a Comment